A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 30, 2019

Muongozaji wa Filamu nguli afariki dunia

Muongozaji mkongwe wa filamu nchini Marekani, John Singleton amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.

Singleton amefariki akiwa na miaka 51 baada ya kulazwa hospitalini kuanzia mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu. Muongozaji huyo anakumbukwa kwa kuongoza filamu zilizopata mafanikio makubwa kama Boyz N The Hood na 2 Fast 2 Furious .

Mapema jana familia yake ilitoa ujumbe kuhusu kumpoteza mpendwa wao.’Tunahuzuni kueleza kuwa John Singleton amefariki dunia, John ametutoka kwa amani akiwa amezungukwa na familia yake pamoja na marafiki’’

Baada ya kifo muandishi na muongozaji huyo wa filamu watu wengi maarufu wakiwemo wasanii wa muziki na waigizaji waliowahi kufanya nae kazi walianza kutoa salamu zao za maomboleza, huku wengi wakimsifu kwa jitiada zake za kuwapa nafasi watu wengi katika kutimiza ndoto zao zakuwa waigizaji wa kubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages