A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, April 15, 2019

RC Makonda Awaasa Wanafunzi kuachana na Mitandao ya kijamii


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaasa wanafunzi kuachana na mitandao ya kijamii badala Yake kuzingatia masomo ili waweza kufikia malengo waliyojiwekea .
Rc Makonda ameyazungumza hayo leo jijini Dar es Salaam na alipokuwa akizungumza  na Wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya  Mzimuni alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi yote iliyopo ndani ya Mkoa huo ambapo ametembelea Shule hiyo kuona ujenzi wa madarasa 6, unaoendelea.
Amesema ili waweze kufanya vizuri katika masomo wanatakiwa kuweka juhudi, nidhamu pamoja na kuheshimu malengo yao waliojiwekea ambapo amewataka wanafunzi hao kufanya vizuri ili Rais Dkt.John Joseph Magufuli kuweza kujivunia  kuzalisha wanafunzi Bora  katika nchi yake.
“Mnauwezo mkubwa Sana wakufanya vizuri achaneni na tabia za kukaa kwenye mitandao ya kijamii wekeni bidii kwenye masomo ili mje kulisaidia Taifa, kuna mambo matatu ukiwa nayo lazima utafanya vizuri unatakiwa kuwa na Juhudi,Nidhamu pamoja na malengo, malengo yako lazima yawe tofauti na Dunia” amesema RC Makonda.
Amesisistiza kuwa wanafunzi wengi wamekiwa wakifuatilia mambo ya dunia Jambo linalopelekea kufanya vibaya Katika masomo, aidha amewataka kuzingatia Yale wanayofundishwa darasani.
Hata hivyo Katika Ziara hiyo RC   Makonda amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Ujenzi ya Scol Construction Ltd iliyotengeneza barabara ya Biafra chini ya kiwango kujisalimisha polisi kabla ya Ijumaa ya April 19.
Itakumbukwa Makonda aliagiza kampuni ya Scol na Delmont kurudia ujenzi wa barabara zilizojengwa chini ya kiwango kwa garama zao zao lakini kampuni ya Delmont imekubali kurudia upya Ujenzi wa barabara ya Mabatini huku kampuni ya Scol" mkandarasi wake akikaidi agizo la kurudia ujenzi wa barabara ya Biafra jambo linaloleta usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri.
Barabara za Mabatini na Biafra zilijengwa na kampuni za Scol na Delmont chini ya kiwango na kuharibika kabla ya kukabidhiwa kwa serikali jambo lililomkwaza RC Makonda na kutaka zirudiwe upya kwa garama ya mkandarasi husika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages