A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, April 15, 2019

RC MAKONDA atoa agizo hili kwa Mkurugenzi Manispaa ya Ilala

RC MAKONDA akizungumza na waandishi wa habari Leo alipofanya Ziara ya kukagua maendeleo ya miradi Katika Wilaya ya Kigamboni

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemtaka Mkurugenzi wilaya ya Ilala, Jumanne Shauri kuhakikisha wanaitisha kikao cha Baraza la Madiwani siku ya Jumanne ili kujadili na kujua tatizo la maradi mingi kukwama katika wilaya hiyo.
RC Makonda ametoa agizo hilo mapema leo alipofanya  ziara maalum, Katika Wilaya ya Kigamboni kata ya Gezaulole, ambapo amepata nafasi ya kukagua ujenzi wa Hospitali, Ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
“Nimeagiza Baraza la madiwani liitishwe kwa dharura kutokana na miradi kukwama ikiwamo machinjio ya vingunguti na ujenzi wa mto msimbazi hivyo nataka kufahamu kwa Nini miradi hiyo inakwama na Katika hii miradi imeshatolewa fedha ila hakuna utekelezwaji” amesema RC Makonda.


Hata hivyo Rc Makonda hakuridhishwa na Kasi ya ujenzi wa jengo la manispaa ya kigamboni Pamoja na nyumba ya mkuu wa Wilaya unafanywa na kampuni ya TPB, ambapo ametaka ifikapo Juni 30 mwaka huu  kukamilisha kama wanavyopaswa.

Aidha amemtaka mkuu wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanaandikishana mkataba kwa upya na kampuni ya TPB inayojenga jengo la manispaa Pamoja na nyumba ya Mkuu wa Wilaya kwamba, Kama jengo halijaisha ifikapo tarehe iliyopangwa wahakikishe wanakabidhi jengo ikiwa Ni Pamoja na kulipa Kodi ya miezi sita.

" Hatuwezi kuwa tunaendelea kukaa kwenye majengo ya kupanga wakati fedha zipo za kukamilisha jengo hivyo DC hakikisha unawaita Hawa watu wa TPB uandikishane nao mkataba Kama hawajakamilisha watatulipa Kodi ya miezi sita Pamoja na kurudisha fedha zitakazobaki za ujenzi" Amesema Makonda.

Aidha Katika Mradi wa jengo la Hospitali ya Wilaya Rc Makonda Amesema anaridhishwa na Kasi ya ujenzi huo ambapo amesema miradi yote hiyo Ni kutokana na kero za wananchi hivyo serikali ipo kwa ajili ya kutatua kero hizo.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya kigamboni Sara Msafiri amemshukuru Rc Makonda kwa kufika kufanya ukaguzi wa miradi hiyo, ambapo kwa upande wake ameahidi kufanya Ziara Mara kwa Mara ili kuona Hali ya ujenzi inavyokwenda.

Nae Mkurugenzi mkuu wa mradi wa TBP mkoa wa Dar es Salaam, Arch Wilison Tesha amebainisha kuwa watahakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa na kuahidi kutekeleza Yale yote yaliyosema na Mkuu wa mkoa alipokagua ujenzi wa majengo hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages