A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, April 15, 2019

RC MAKONDA AFANYA ZIARA WILAYA YA KINONDONI AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MIRADI MBALIMBALI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya zira ya kikazi ya kukagua miradi  Wilaya ya Kinondoni miradi inayotekelezwa na Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (wapilikushoto) akisalimiana na mmoja ya viongozi wanaosimamia ujenzi wa soko la Magomeni wakati alipofanya ziara yake yakikazi yakukagua na kutembelea miradi mbalimbali, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  akimsikiliza mmoja wa kiongozi wanaosimamia ujenzi wa soko la Magomeni wakati alipofanya ziara yake yakikazi yakukagua na kutembelea miradi mbalimbali.
Baadhi ya Wafanya kazi wakiwajibika katika ujenzi wa soko hilo.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kushoto)akimsikiliza Mganga mkuu wa Manispaa ya kinondoni Dk. Festo Dugange wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kutembelea miradi na ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa kata ya Kigogo .







 Mkuu wa Mkoa Paul Makonda   akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo. wakati wa ziara hiyo.




Mkuu wa Mkoa akizungumza wakati alipotembelea ujenzi wa Barabara ya Mburahati barafu.

Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda akikagua ujenzi wa barabara ya  Tandale  kwa Mtogole




Mkuu wa Mkoa akiwa barabara ya SIMU2000 Mawasiliano.

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akikagua barabara  ya Sinza Mabatini 

Mkuu wa mkoa wa Dar es Paul Makonda amefurahishwa na Kasi ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Katika Wilaya ya kinondoni ambapo mpaka kufikia Sasa utekelezaji wake unaenda vizuri.

Ikiwa Ni mwendelezo wa Ziara yake, Leo April 15, RC Makonda ametembelea miradi mbalimbali Katika Manispaa ya Kinondoni ambapo lengo la Ziara hiyo Ni kuona Kasi ya utekelezwaji wa ujenzi Katika miradi hiyo ambayo ni miradi Katika sekta ya Afya, Barabara ambayo imetolewa fedha kutoka Katika Serikali.

Makonda ametembelea ujenzi wa Soko la Magomeni,ujenzi wa kituo Cha Afya kigogo ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibunii, Soko la Sinza, Pamoja na ujenzi wa Barabara ya Barafu Mbulahati,  ambapo amewataka wakandarasi kufanya kazi zao kwa kuzingatia ueledi.

Amesema wakandarasi wamekuwa wakifanya kazi bila kuzingatia viwango Jambo linalopelekea barabara kuwa mbovu baada ya muda mchache, ambapo amesema wapo waliofungiwa kufanya kazi Katika mkoa huo, na wengine kutakiwa kurudia ujenzi wa barabara kwa fedha zao wenyewe.

Aidha amemtaka Mkuu wa Wilaya ya hiyo kuhakikisha anaendelea kusimamia kikamilifu miradi yote ili iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa na kuweza kutatua kero na adha zinazowakumba wananchi.


Pia amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kushughulikia changamoto za malipo kwa wa Vibarua rwanaofanya kazi katika miradi hiyo huku akiweka sawa mailpo halali wanayotakiwa kulipwa kuwa ni kiasi cha shilingi 12,500 na si chini na hapo.
“Tuna matumaini makubwa sana kutokana na kasi wanayoenda nayo na nampongeza sana DC kwa kazi anayoifanya, barabara ya kituo cha simu 2000 pia inaendelea vizuri na kuna kipande cha mita 250 kimechukuliwa na TANROADS kwa jailli ya kuunganisha na ujenzi wa barabara ya Ubungo hivyo wananchi wakiona kinachelewa wasijiulize kwa Nini hii Ni kwamba tunataka kuunganisha na ujenzi wa barabara ya juu inayojengwa ya Ubungo" Amesema Rc Makonda.
Ziara ya kukagua miradi ndani ya Mkoa huo bado zinaendelea ambapo siku ya kesho RC Makonda ataendelea na ziara katika wilaya ya Kinondoni

MATUKIO KATIKA PICHA
















No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages