Manchester United inaweza kupata ushindi dhidi ya Barcelona wakiwa ugenini, kocha wa Mashetani Wekundu hao Ole Gunnar Solskjaer anaamini.
Barca wameifunga United 1-0 katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dimbani Old Trafford, goli la Barcelona limepatikana katika dakika ya 12 baada ya mlinzi wa United Luke Shaw kujifunga, Mchuano wa marudiano utafanyika dimbani Nou Camp Jumanne wiki ijayo.
"Tunacheza na timu kubwa sana. Ni timu ngumu - tutaenda nyumbani kwao tukijua kuwa tutaweza kushinda kule," Solskjaer amekiambia kituo cha runinga cha BT Sport.
"Tunaenda kule tukiwa na kitu kimoja tu kichwani: tunatakiwa kushinda."
Katika hatua ya mtoano, United walionekana kana kwamba wameshayaaga mashindano baada ya kupoteza kwa goli 2-0 dhidi ya Paris St-Germain wakiwa nyumbani, lakini wakawaacha watu midomo wazi baada ya kwenda kupata ushindi wa 3-1 nchini Ufaransa, na kufanikiwa kuendelea kwa faida ya goli magoli la ugenini.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, April 11, 2019
Ole Gunnar Solskjaer ana hakika kuwa United inaweza pata ushindi ugenini
Tags
MICHEZO#
Share This
About kilole mzee
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment