A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 30, 2019

KONGAMANO LA KIMATAIFA LA QNET LAWALETA PAMOJA WAJASIRIAMALI 13,000 PENANG


Wageni waheshima wa QNET, Maofisa wa Malaysia na wageni wa heshima waalikwa wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa kongamano la siku tano la QNET lililofanyika jijini nchini Malaysia. Zaidi ya wajasiriamali 13,000 waliudhuria kwenye maonyesho hayo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa QNET na Wageni wa heshima wakiwa wamepozi pamoja mara baada ya kukata utepe wa uzinduzi wa kongamano la siku tano la QNET.
Penang, Tarehe 23 Aprili 2019 - Kampuni maarufu ya kimataifa yenye asili ya Asia ya mauzo ya moja kwa moja, QNET inaendesha kongamano la siku tano la kimataifa ambalo linaleta pamoja takribani wajasiriamali 13,000 kutoka maeneo mbalimbali duniani katika kisiwa cha Penang

Kongamano lenye hamasa litashuhudiwa na wasambazaji wa QNET kutoka katika zaidi ya nchi 30 watakao kutana pamoja katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa na maonyesho wa Subterranean Penang International Conference & Exhibition Centre (SPICE) katika mji wa Bayan Baru, Penang, Malaysia

Shughuli za ufunguzi wa sherehe zilifanywa na Yang Berhormat Profesa Dr. P. Ramasamy, Naibu Waziri Kiongozi II wa Penang, Mwenyekiti Mtendaji wa QI Group, Dato Sri Vijay Eswaran na Kaimu Naibu Mwenyekiti Joseph Bismark. Vile vile walikuwepo Mh. Cissé Ibrahim Sory, Meneja Mkuu wa Guinea Microfinance Agency ANAMIF, na washirika wengine wa biashara za kimataifa wa QNET kutoka Afrika, na sehemu mbalimbali duniani.

Kongamano hili ambalo linajulikana kama V-Malaysia 2019 limefanyika Penang kwa miaka sita mfululizo. Wateja na wasambazaji kutoka katika masoko makubwa ya kikanda ya QNET katika Mashariki ya Kati, Katikati ya Asia, Afrika, Bara Hindi, Indonesia na Malaysia wanahudhuria kongamano la mwaka huu. Kongamano la siku tano litajumuisha mfululizo wa programu za mafunzo, hotuba za uhamasishaji, kutambulisha bidhaa mpya za mtindo wa maisha wa QNET na burudani. Kivutio kikubwa mwaka huu ni QNET Carnival ambayo itaonyesha zaidi ya nembo au lebo 50 za bidhaa za QNET katika moja ya maonyesho makubwa kuwahi kufanywa na kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages