A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 26, 2019

Kimbunga Kenneth kusababisha maafa zaidi nchini Msum


Kimbunga Kenneth kimepiga pwani ya kaskazini ya Msumbiji usiku wa Alhamis huku mvua kubwa zikitarajiwa mara mbili zaidi ya dhoruba iliyoupiga mji wa Beira mwezi uliopita. Mtu mmoja amefariki huku makazi yakiharibiwa.

Kimbunga Kenneth kimelipiga jimbo la Cabo Delgado, kisha baadae kikaelekea jimbo la Sofala kaskazini mwa Msumbiji ambako ndiko uliko mji wa Beira ulioathiriwa zaidi na kimbunga Idai mwezi uliopita, Kimbunga Idai kiliwaua mamia ya watu na kusababisha maelfu kukosa makazi nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.

Kwa mujibu wa shirika la Mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP, kimbunga Kenneth kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa katika kipindi cha siku 10 zijazo ikiwa ni mara mbili zaidi ya zile zilizonyesha wakati wa kimbunga Idai.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages