Wafanyakazi wa Kampuni ya ujenzi ya China (Chec), wamegoma kufanya kazi wakishinikiza iwapatie mikataba yenye masilahi bora ikiwamo nyongeza ya mishahara na marupurupu mengine.
Mgomo huo umehusisha wafanyakazi wa kada mbalimbali ambao kwa pamoja wanalalamikia matatizo yanayofanana.
Wameilalamikia kampuni ya Vipaji Link ambayo inashughulikia rasilimali watu katika kampuni ya Chec kwamba inawahujumu.
Akizungumzia mgomo huo leo, Jumatatu, Machi 18 mjumbe wa chama cha wafanyakazi wa kampuni hiyo kiitwacho Tasiw, Suleiman Omary amesema hawautaki mkataba wa zamani kwa sababu hauna masilahi kwao na kwamba mwajiri wao amekuwa haufuati.
“Kwa kifupi sisi tunataka mkataba wenye hali bora ambao utakuwa na mambo manne ambayo ni mshahara mzuri wa mfanyakazi, hela ya chakula, hela ya matibabu na usafiri,” amesema Omary.
Pia amesema wanataka pia kampuni ya Vipaji Link iondoke kwa sababu wamekuwa wakifanya kazi kama madalali kati ya Wachina na wafanyakazi, jambo ambalo wanadai linadumaza masilahi yao.
No comments:
Post a Comment