A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, March 22, 2019

RC Makonda atoa siku tano kwa DC Ilala, Kinondoni

Kufuatia kusuasua kuanza kwa miradi ya kimkakati, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewaagiza Wakuu wa Wilaya za Ilala na Kinondoni, Wakurugenzi wa manispaa na wakuu wa idara kuhakikisha hadi kufikia Jumanne ya March 26 miradi yote iwe imeanza utekelezaji ikimaanisha kuwa mikataba imesainiwa na mkandarasi yupo kazini.

RC Makonda amefikia hatua hiyo baada ya kuchukizwa kuona miradi haijaanza kutekelezwa hadi sasa licha ya Rais Dkt. John Magufuli kutoa fedha zote za miradi lakini baadhi ya watendaji wamekuwa wakichelewesha kuanza kwa miradi.

Aidha RC Makonda amempa Siku tatu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema na Mkurugenzi wa manispaa hiyo kuhakikisha mkataba wa ujenzi wa machinjio ya kisasa Vingunguti unasainiwa mara moja na mkandarasi anaanza kazi.

Hivyohivyo RC Makonda amempa siku tano Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Mkurugenzi wake kuhakikisha ujenzi na Maboresho ya ufukwe wa kisasa wa Coco unaanza mara moja.

Makonda amesema endapo wahusika watashindwa kutekeleza agizo hilo watatafsiriwa kuwa wameshindwa kusimamia fedha na miradi ya serikali.

Itakumbukwa mwaka jana Rais Dkt.John Magufuli alitoa fedha za kutosha kwaajili ya miradi ya kimkakati ya kuwakwamua wananchi ikiwemo ujenzi wa barabara, hospital, zahanati,vituo vya daladala,maji,umeme,elimu na machinjio ili kupunguza kero za wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages