Afisa
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Grace Mgaya, akizungumza wakati wa kutangaza fursa ya kipekee kwa wadau wa tasnia ya filamu Tanzania na barani afrika hafla yakutangaza fursa hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Uhusiano MultiChoice
Tanzania, Johnson Mshana akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya
MultiChoice Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli ya Southern
Sun mapema leo asubuhi.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu Tanzania Mama Joyce Fisoo akizungumza wakati wa uzinduzi wa
programu ya MultiChoice Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli
ya Southern Sun mapema leo asubuhi.
Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana akizungumza na Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Mama Joyce Fisoo akizungumza
wakati wa uzinduzi wa programu ya MultiChoice Talent Factory portal
iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun mapema leo asubuhi.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu Tanzania Mama Joyce Fisoo akiwa na Afisa Uhusiano MultiChoice
Tanzania, Grace Mgaya wakati wa uzinduzi wa programu ya MultiChoice
Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli ya Southern Sun mapema
leo asubuhi.
Baadhi ya picha zikionyesha
baadhi ya wadau na waigizaji wa filamu walioalikwa kwenye uzinduzi wa
programu ya MultiChoice Talent Factory portal iliyofanyika katika hoteli
ya Southern Sun mapema leo asubuhi.
Jumanne Machi
19, 2019:MultiChoice Tanzania imetangaza
fursa ya kipekee kwa wadau wa tasnia ya filamu Tanzania na barani Afrika
kwa ujumla ijulikanayo kama MultiChoice Talent Factory Portaliliyodhamiria
kuleta mapiduzi ya hali ya juu katika uaandaaji wa filamu zenye viwango vya
kimataifa kutoka barani Afrika.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano kutoka
MultiChoice Tanzania Johnson Mshana alieleza kuwa programu hiyo ni muendelezo
wa program maalum ya iliyodhamiria kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu barani
Afrika. “MultiChoice Talent Factory ambayo ni progamu mama ilizinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka
jana naimedhamiria kuleta mabadiliko chanya kwenye tasnia ya filamu hapa
nyumbani Tanzania na Afrika kwa ujumla. Tulianza kwa kupeleka vijana wanne
katika kambi maalum ya mafunzo ya uandaaji filamu katika akademia maalum kule
Nairobi nchini Kenya, kisha mafunzo maalum kwa magwiji wa sauti yaliyofanyika mnamo
mwezi Januari mwaka huu na hatimaye leo hii tumekuja tena na platform maalum yenye
dhamira ile ile ya kuleta mapinduzi katika tasnia ya filamu
barani Afrika”, alisema Mshana.
Kwa upande wake
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi Joyce Fisoo alisema kuwa,
anaishukuru sana kampuni ya MultiChoice kwani imekuwa mstari wa mbele katika
kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu hapa nyumbani Tanzania. “Binafsi nilishuhudia uzinduzi wa programu
ya MultiChoice Talent Factory mapema mwaka jana kule mjini Dodoma na leo hii
tunazindua tena sehemu nyingine ya programu hiyo hiyo. Hakika ni fursa ya
kipekee na ninapenda kuchukua nafasi hii kuwahamasisha wadau wote waliopo
katika Tasnia yetu kuitumia nafasi hii ipasavyo ili kuweza kujifunza,
kubadilishana ujuzi na hatimaye kupata kazi zenye maudhui ya hali ya juu kutoka
hapa hapa Afrika”, alisema Mama Fisoo.
Naye Afisa
Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Grace Mgaya alimalizia kwa kueleza kuwa
ukurasa huu wa ni wa wazi kwa watu wote hususani wadau wa filamu waliopo hapa
nyumbani na Afrika kwa ujumla. “Tunaamini
kwa kupitia program hii tutaweza kuwafikia wadau wengi zaidi na tunatarajia
kazi zenye ubora wa hali ya juu kutoka barani Afrika kwa siku zijazo kutokana
na matokeo chanya yatakyoletwa na program hii ya MultiChoice Talent Factory”,
alisema Grace.
No comments:
Post a Comment