A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 16, 2019

KAULI YA RC MAKONDA YARUDISHA MATUMAINI YA KIJANA HAMISI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimjulia hali Kijana Hamis Hashim, alipokwenda kumtembele Hospitali ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la Miguu kuvimba leo hospitalini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi kiasi cha Shilingi laki tano Kijana Hamis Hashim, kwaajili ya kununulia chakulas kipindi amabacho atakuwa Hospitali akipatiwa matibabu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt Ibrahim Nkoma, Mkuu wa Mkoa alipokwenda kumjulia hali Kijana Hamis Hashim,
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda (wapilikulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Algaesha, mara baada ya Mkuu wa Mkoa alipotoka kumjulia hali Kijana Hamis Hashim, wengine pichani ni baadhi ya wasanii walioongozana na Mkuu wa Mkoa wakiongozwa na Stive nyerere pamoja na Madaktari wa hospitali hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda leo amemtembelea na kumjulua hali
kijana Hamis Hashim alielazwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la Miguu kuvimba hadi kuzidi uzito wa mwili ambapo ameahidi kusaidia gharama za matibabu iwe ndani au nje ya nchi hadi atakapopona.
 
RC Makonda baada kuona taarifa za kijana Hamis kapitia mitandao ya kijamii aliguswa na kuona anao wajibu wa kumsaidia ambapo juzi aliagiza apelekwe hospital ya Muhimbili kwaajili ya kuchukuliwa vipimo ambapo licha ya Hamis kuugua pia anaishi katika Familia ya hali ya chini akimtegemea Mama mzazi ambae nae hana kazi baada ya Baba mzazi kufariki.

 
Aidha RC Makonda amesema kwa sasa hali ya Afya ya Hamis inaendelea vizuri baada ya madaktari bingwa wa Muhimbili kuendelea kuchukuwa vipimo kwa umakini wa hali ya juu.

 
Pamoja na hayo RC Makonda amemkabidhi Kijana Hamis kiasi cha Shilingi Laki Tano kwaajili ya Kununua chakula kwa siku atakazokuwa Hospital.

 
Kwa upande wake Hamis Hashim amemshukuru RC Makonda kwa moyo wa huruma aliokuwa nao ambapo ameeleza kuwa amekuwa anaishi maisha ya tabu lakini kwa sasa anajisikia faraja kuona RC Makonda ameahidi kumsaidia kwa kila jambo.

 
Kwa Mujibu wa Dr. Ibrahim Nkoma ambae ni Mkuu wa idara ya upasuaji hospital ya taifa Muhimbili anasema Hamis Hashim anasumbuliwa na tatizo la neva za fahamu kukuwa kupita uwezo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages