A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, February 20, 2019

RPC Mwanza kula sahani moja na wahalifu


Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, Muliro Muliro ameahidi kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu, ukiwemo ujambazi wa kutumia silaha.

Kamanda Muliro ametangaza vita dhidi ya wahalifu sugu mkoani Mwanza, wakati wa tukio la kumuaga aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoani humo Kamishna msaidizi wa polisi Jonathan Shanna ambaye amehamishiwa makao makuu ya Jeshi la polisi Tanzania kitengo cha operesheni maalum za jeshi hilo.

Aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Jonathan Shanna ambaye amehudumu kwa miezi sita akatoa rai ya kumpa ushirikiano kamanda huyo mpya katika kukomesha uhalifu wa nchi kavu, majini na barabarani. Tukio lililofanyikia kwenye uwanja wa polisi Mabatini jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages