Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa ameamua kujizulu nafasi yake ya usuluhishi wa mgogoro wa
Burundi kwa kile alichokidai kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kushindwa kuunga mkono
jitihada za kumaliza mgogoro huo.
Ameelezea masikitiko yake na hatua ya serikali ya Burundi kususia kikao cha mwisho cha
mazungumzo na hali hiyo inaonyesha msimamo wa muda mrefu wa viongozi wa Burundi wa kutoshiriki katika mazungumzo baini ya Warundi.
Pia ameeleza kusikitishwa kuona hakuungwa mkono vya kutosha katika jitihada zake, kwanza na Jumuiya ya Afrika Mashariki:
"kutofanyika kwa mkutano wa kilele kuhusu mgogoro wa Burundi ulisababisha mimi kukosa uungwaji mkono wa jumuiya," amesema Rais Mstaafu wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment