Leo Bungeni Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuna haja ya kusimamisha Mshahara na Malipo yote ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu hadi pale atakapopata taarifa rasmi alipo mbunge huyo na nini anafanya.
Kauli hiyo ya Spika imekuja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku (Musukuma) kuomba muongozo wa Spika kuhusu Tundu Lissu kutokuwepo Bungeni.
"Tunaona Mhe. Tundu Lissu anazunguka kwenye nchi mbalimbali lakini huku anasomeka kama mgonjwa. Sasa Mh. Spika nilikuwa naomba muongozo wako, ni lini Bunge litashitisha mshahara wake kwa kuwa ameshapona anazurusa na Bunge linaendelea na yeye hayupo," amesema Musukuma.
Alichojibu Spika Ndugai
Kwa maana kwamba Mbunge hayupo jimboni kwake, hayupo hapa bungeni tunapafanya kazi, hayupo hospitalini, hayupo Tanzania.
Na taarifa zake spika hana kabisa wala hajishughulishi kumwandikia Spika kumwambia nipo sehemu fulani nafanya hivi na kama ni mgonjwa hakuna taarifa yoyote ya Daktari ipo haja ya kusimamisha malipo ya aina yoyote ile mpaka hapo tutakapopata taarifa yupo wapi na anafanya nini.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, February 7, 2019
MSHAHARA WA TUNDU LISSU KUSITISHWA BUNGENI
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment