Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Malipo ya wakulima wa korosho sasa yamefikia TSh. Bilioni 524.8 baada ya Serikali jana kuwalipa wakulima cha Tsh. Bilioni 100.
Ameeleza hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma leo, kipindi kinachofanyika kila alhamisi.
"Tunaendelea kufanya uhakiki na mpaka jana tumeongezewa Bil.100 ambazo zinafanya jumla ya Bil.500 za kulipa. Tutahakikisha hadi tarehe 15 mwezi huu tutakuwa tumewalipa wakulima kwa kiasi kikubwa,” amesema Waziri Mkuu.
Awali Waziri Mkuu alisema kuwa serikali inaendelea na mkakati wa kupanua wigo wa biashara kwa kupanua sekta zinazowasaidia wafanyabiashara kufanya vizuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa ndege.
No comments:
Post a Comment