A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, February 4, 2019

Kocha wa Yanga SC awafungukia TFF


Kocha Mkuu wa timu ya Yanga SC, Mwinyi Zahera amelishutumu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa namna walivyopanga ratiba ya mechi za ligi.

Kocha huyo ameyasema hayo mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga na kumalizika kwa mabao 1-1 kuwa ratiba haiko haipo sawa.

Ameeleza kuwa awali TFF waliwapangia kucheza mechi nyingi nyumbani wakiwa na malengo mabaya dhidi yao ambapo sasa wana mechi nyingi za ugenini.

"Ratiba si rafiki kwetu, tuna mechi nyingi za ugenini kwa sasa, wachezaji wanasafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na wanachoka, vema TFF wakalitazama upya hili.

Zahera amewataka viongozi wa TFF kuangalia upya suala hili la sivyo linaweza kuwa sehemu ya soka la Tanzania kupotea.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages