Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo akihutubia
mkutano maalumu unaofanyika mjini Geneva Uswisi kuhusu udhibiti wa
silaha amesema maono mapya ya kimataifa ya udhibiti wa silaha
yanahitajika na nchi hazipaswi "kulala" katika mbio mpya ya silaha za
nyuklia.
Guterres ameeleza kuhusu vitisho kadhaa dhidi ya usalama wa dunia
kutokana na kuenea kwa silaha akitolea mfano silaha za kemikali, silaha
zinazojiendesha zenyewe na kuweza kushambulia kwa kadri zilivyoelekezwa
kwa mfumo wa komputa na pia silaha za masafa marefu.
Maoni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yamekuja siku chache kabla ya
mkutano wa pili kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kim Jong-un wa
Korea kaskazini.
Guterres amesema, “maelfu ya maisha ya raia yanaendelea kupotea
kwasababu ya matumizi haramu ya silaha ndogondogo na matumizi ya silaha
za uwanja wa vita katika miji.
Amesema miaka 70 iliyopita imeshuhudia maendeleo makubwa katika juhudi
za udhibiti wa silaha, Guterres amesisitiza, akisema kuwa zile
zilizofanikiwa zaidi ni zile zilizoongozwa na “nguvu kubwa” lakini
mafanikio hayo yako hatari kutokana na aina mpya ya silaha.
Akielezea hatari ya kuruhusu kukoma kwa mkataba wa udhibiti wa silaha
uliofikiwa kati ya Marekani na Urusi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Guterres ameonya kuwa nchi za Ulaya zitakuwa miongoni mwa nchi za kwanza
ambako ukosefu wa usalam utahisiwa zaidi.
Guterres amesisitiza, “juhudi zinatakiwa kufanyika ili kuongeza mwanzo
mpya wa mkataba kati ya Marekani na Urusi kabla haujafika mwisho wake
mwaka 2021.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, February 27, 2019
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: Dunia isilale katika udhibiti wa silaha
Tags
KIMATAIFA#
Share This
About kilole mzee
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment