A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 19, 2019

Fei Toto apiga hesabu za Ubingwa Yanga SC

Kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amesema hawajakatishwa tamaa na matokeo 
waliyoyapata ya kufungwa na Simba sc na badala yake wataendelea kupambana kuhakikisha
wanafanya vizuri katika michezo inayofuata ya ligi.

Fei Toto alisema Simba walitumia vyema nafasi moja waliyoipata na kufanikiwa kupata ushindi
huo walioupata.

“Hatukati tamaa, tutaendelea kupambana, niwaombe mashabiki waendelee kutusapoti ili
tupate matokeo mazuri,” ameeleza Fei Toto.

Ameendelea kwa kusema, 'kikubwa tunajipanga kwa ajili ya michezo ijayo ya ligi na kikubwa
tunataka kuona timu ikiendelea kuongoza ligi na mwishoni mwa msimu tuchukue ubingwa'.

Licha ya kipigo kutoka kwa Simba SC hapo Jumamosi, Yanga SC bado inaongoza Ligi Kuu
Soka Tanzania Bara ikiwa imejikusanyia pointi 58 katika michezo 24 ya Ligi waliyocheza hadi sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages