A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 19, 2019

Diamond alitusaidia kuibadili kauli mbiu wakati wa kampeni - January Makamba


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano, January Makamba amesema kuwa msanii Diamond Platnumz alisaidia kupatikana kwa kauli mbiu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2015.

Amebainisha hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachoruka Clouds TV ambapo ameeleza kuwa Diamond alibadilisha kutoka Hapa Ni Kazi Tu hadi kuwa Hapa Kazi Tu.

"Msanii Diamond Platnumz alitusaidia kuibadili kauli mbiu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015 kutoka Hapa Ni Kazi Tu, na kuwa Hapa Kazi Tu," amesema.

Ameendelea kwa kueleza, 'Alipoiona tu mezani alisema, mtaani hatusema Hapa Ni Kazi Tu, bali tunasema Hapa Kazi Tu,'.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages