Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa China Nchini, Mhe. Wang Ke wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Kutoa Tuzo za Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI, Desemba 5, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini katika bango wakati alipowasili kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam kutoa Tuzo za Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI, Desemba 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika sherehe za Utoaji Tuzo za Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Desemba 5, 2018. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Atashasta Nditiye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya HUAWEI nchini, Frank Zhou na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Tuzo Mshindi wa Kwanza wa Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI, Emmanuel Chaula wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika sherehe za kukabidhi Tuzo hizo kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Desemba 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokabidhi Tuzo za Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Desemba 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Viongozi wa Kitaifa na Kimataifa wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI baada ya kuwakabidhi tuzo za ushindi washindi hao kwenye hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam, Desemba 5, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke (wapili kulia) na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipotoka kwenye ukumbi wa hoteli ya Hayyat Regency jijini Dar es salaam baada ya kutoa Tuzo kwa washindi wa Mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI, Desemba 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment