Baada ya dirisha dogo la usjili kufungwa juzi Desemba 15 Wanachama na mashabiki wa Simba na Yanga katika maeneo tofauti wamefunguka na kutoa maoni yao husu usajili huo.
Mmoja wa Wanachama kutoka tawi la Umoja Tandale kwa Mtogole amesema kuwa Yanga hawajafanya usajili wamepewa Wachezaji, kwasababu usajili niule Mwalimu aliouhitaji na huo ndio wao wanaoutaka.
" Sisi Wanachama wa Yanga tunasema hatujafanya Usajili ukisema Yanga wamefanya usajili niule Mwalimu aliouhitaji huo ndo usajili tunasema umefanyika ma mdio tunaoutaka sisi kama tumepewa Wachezaji Mwalimu anafalsafa yake anamuitaji fulani na fulani wewe Kiongozi mwisho wa siku hamna Wachezaji hao maana yake ujafanya usajili" alisema Mwanachama huyo
Nae Shabiki wa Simba kwa upande wake amesema kuwa Kocha amefanya jambo zuri kwa kumuongeza Beki mpya Zana kwasababu amekuja kuongeza nguvu kwani Shomari Kapombe ni majeruhi.
" Mimi naamini Mwalimu yupo na ameona wapi kunamapungufu ndipo alipohitaji aongeze nguvu na kumuongeza beki mpya Zana kwani ikizingatiwa Shomari Kapombe ni majeruhi kwahiyo Kocha amefanya kazi yake" alisema Shabiki huyo
No comments:
Post a Comment