A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, December 19, 2018

Baada ya Mourinho kutimuliwa, Solskjaer kuchukua mikoba?

Ole Gunnar Solskjaer

Mpaka sasa bado hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kama raia huyo wa Norway atachukua mikoba ya Jose Mourinho ambaye alifutwa kazi jana Jumanne.

Hata hivyo taarifa iliwekwa kwenye tovuti ya klabu hiyo ikisema mshambuliaji huyo wa zamani wa United ni "kocha wetu wa muda". Taarifa hiyo hata hivyo ilifutwa baadae.

Solskjaer, mwenye miaka 45 sasa, ameifungia United magoli 126 katika misimu 11 chini ya kocha Sir Alex Ferguson.

Pia alishinda makombe sita ya ligi ya Premia, mawili ya FA na moja la Klabu Bingwa Ulaya.

Kwa sasa anafundisha klabu ya Norway ya Molde lakini msimu wao wa mwaka 2018 umesitishwa kupisha majira ya baridi kali na mechi zitarejea mwezi Machi mwakani.

Video inayomuonesha Solskjaer akifubga goli la ushindi katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich mwaka 1999, iliwekwa kwenye tovuti ya United na kuambatanishwa na maelezo kuwa: "Solskjaer anakuwa kocha wetu wa muda, misimu 20 baada ya kushinda makombe matatu kwa mpigo na LILE goli lake katika (uwanja wa) Camp Nou..."

Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg alipokea taarifa hiyo kwa furaha na kuandika katika ukurasa wake wa twitter: "Siku njema kwa mpira wa Norway. Nakutakia mema katika kuongoza Mashetani Wekundu." Hata hivyo aliufuta ujumbe huo baadae.

Mechi ya kwanza ya Solskjaer kama atakabidhiwa mikoba itakuwa dhidi ya Cardiff City siku ya Jumamosi. Kocha huyo aliifundisha Cardiff hapo awali na kushuka nao daraja mwaka 2014.

United wanatarajiwa kumchagua kocha mpya mwisho wa msimu. Tayari majina matatu ya Zinedine Zidane na Waagerntina wawili Diego Simeone na Mauricio Pochettino yamekuwa yakipigiwa upatu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages