A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, December 16, 2018

GEITA GOLD YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA MWAJIRI BORA 2018

Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jane Nyimbo akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa katika hafla ya kutoa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na chama hicho katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akiwa mgeni rasmi ilitoa tuzo kwa kutambua vipengele 17 kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji Tuzo kwa Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo Mh. Anthony Mavunde (MB), Mhe. Stella Ikupa (MP), wawakilishi wa balozi za Norway, Denmark, China  pamoja na taasisi mbali mbali ikiwemo TUKTA, ILO, na waajiri mbali mbali.

Mwakilishi kutoka kampuni ya utengenezaji Sigara  (TCC), akiwa amebeba Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya tatu katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB).

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) wapili (kulia) akikabidhi tuzo kwa Mwakilishi wa kampuini ya Bia Tanzania  (TBL), Lilian Makau wakati wakutoa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya Kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya pili katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa ATE Jane Nimbo watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho Dk. Aggrey Mlimuka.
Wafanyakazi wa Geita Gold Mine (GGM) wakifurahiya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) baada ya kampuni hiyo kuibuka kidedea nakushika nafasi ya kwanza  kwenye Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018e  hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani.
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Disemba 14 2018 kimeandaa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka
2018 zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Tangu kuanzishwa kwake
mwaka 2005, tuzo hizo zimejikita katika kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa
nguvu kazi na rasilimali watu kwa lengo la kuwawezesha kutimiza wajibu wao kikamilifu na
kupelekea kukuza uzalishaji wa kibiashara. Tuzo hizo zilihudhuriwa na wadau mbali mbali
wakiwemo Mh. Jenista Mhagama, Mh. Anthony Mavunde, Mhe. Stella Ikupa, Mkuu wa Mkoa
DSM, Mhe. Paul Makonda, Balozi wa Norway nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Denmark
nchini, Bw. Einer H. Jensen na Balozi wa China nchini Nd. Wang Fe, pamoja na taasisi mbali
mbali ikiwemo TUKTA na ILO.

Tuzo hizo zinazofanyika kila mwaka zimasaidia kuhamasisha wanachama kuchukulia masuala
ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama misingi muhimu katika kumwezesha mwajiri kuwa
na wafanyakazi wenye uwezo na ueledi ili kukidhi mahitaji ya ushindani katika biashara.
Sherehe ya utoaji tuzo iliyohudhuriwa na Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa Mgeni Rasmi, zimekuwa
maarufu hapa nchini katika muktadha wa biashara hasa kwa kuhamamasisha makampuni
makubwa na madogo na ya ukubwa wa kati kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya
kufanya biashara nchini.

Tuzo hizo ambazo kwa mwaka 2017 ziliboreshwa kwa kuongezewa vipengele 12 vipya vya Hali
nzuri kwa Wafanyakazi (Employee Wellness), Kuvutia na kutunza wafanyakazi wenye ujuzi
(Attraction and Retention), Mahusiano Mazuri Mahali pa Kazi (Industrial Relations), Kujali kazi na
maisha nje ya Kazi (Work Life Balance), Mwajiri anayekubalika na Kufahamika (Employer
Branding), Usimamizi wa Wafanyakazi kwa kuzingatia Umri (Managing an Aging Workforce),
Uwekezaji katika Teknolojia (Technology Investment), Tuzo kwa ajili ya Sekta Binafsi (Private
Sector Award), Tuzo kwa Sekta ya Umma (Public Sector Award), Tuzo kwa Ajili ya Mashirika ya
Kijamii ( Civil Society Award) na Tuzo ya Mwajiri Mzawa (Indigenous Employer Award) ,
zitaendelea na vipengele hivyo vipya kwani vinatoa fursa kwa wanachama kufanyia kazi
vipengele hivyo kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi na ajira kulingana na mahitaji ya
waajiri nchini.

Akizumgumza na wageni waalikwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu alisema kwamba
serikali inatambua mchango wa waajiri kutoka sekta zote na itaendelea kushirikiana nao
pamoja na Vyama vya Wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika kutimiza azma ya nchi yetu
kujitegemea. Mhe. Jenista Mhagama aliongeza kuwa serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania, Dr. John Joseph Magufuli imebeba jukumu la kuboresha
miundombinu katika nyanja za usafirishaji wa anga, reli na maji, afya, nishati, elimu na
mawasiliano ambayo kwa kiasi kikubwa zinaongeza uzalishaji wa nchi kupitia waajiri wa sekta
binafsi na umma.

Aidha Mh. Mhagama alipongea Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa shughuli zake mbali
ikiwemo Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Uongozi kwa Mwaka
2018, Mwanamke wa Wakati Ujao inayofanyika kwa ushirikiano na Shirikisho la Vyama vya
Waajiri nchini Norway (NHO) kutoa mafunzo kwa wanawake ili waweze kushika za juu za
uongozi katika makampuni na taasisi mbali mbali ambapo tangu kuasisiwa kwake mwaka 2016,
wanawake 66 wamehitimu mafunzo hayo.

Akiongea na wageni waalikwa, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jayne
Nyimbo Taylor alishukuru serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zake katika kuboresha
mazingira ya kufanya biashara nchini kama punguzo la tozo inayolipwa na waajiri kwa ajili ya
kukuza ujuzi mahali pa kazi maarufu kama “Skills Development Levy (SDL)” kutoka 6% mpaka
kufikia 4.5% huku akiiomba serikali kuipunguza tozo hiyo hadi kufikia 2%. Pamoja na
mapendekezo hayo, Bi. Jayne Nyimbo pia aligusia changamoto mbali mbali zinazowakabili
waajiri kama ufuatiliaji wa vibali vya kufanya kazi nchini, utaratibu wa malipo ya Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo sekta binafsi wanalipa 1% huku waajiri wa umma wanalipa
0.5% ya mshahara anaolipwa mfanyakazi, aina mikataba ya ajira pamoja na tozo na faini
zinazotozwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).

Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania(ATE), Dkt.
Aggrey K. Mlimuka, alitoa shukrani zake za dhati kwa Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, wageni
waalikwa na wadau mbali mbali waliofanikisha Tuzo ya Mwajiri wa Mwaka 2018. “Naomba
nikushukuru tena Mhe. Mgeni Rasmi, na Washiriki wote kwa kuja kujumuika na sisi katika utoaji
wa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018, na naamini kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa
kushikiana na TUCTA pamoja na Serikali hasa tunapoendelea kujenga nchi yetu kuelekea
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Naomba kutumia fursa hii pia kuwashukuru na
kuwapongeza wanachama wote walioshiriki katika zoezi hili hasa kwa kujaza dodoso ili kupata
fursa ya kulinganisha utendaji wa makampuni yao na ya wengine.” Alisema Dkt. Mlimuka.
“Naomba kuhitimisha salamu zangu kwa kuwatambua uwepo wa baadhi ya wanachama na
wadau wetu kwa michango yao ambayo imetuwezesha kufanikisha utoaji wa tuzo hii ambao ni
wafuatao.” Alimalizia Dkt. Mlimuka.

Kuhusu Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ni chombo pekee cha waajiri kinachowawakilisha vema
nchini Tanzania. Kiliundwa mwaka 1960 ili kusimamia na kulinda maslahi ya waajiri katika
masuala ya kazi na ajira.

Kama sauti muhimu ya masuala ya kibiashara, Chama cha waajiri Tanzania kinawakilisha waajiri
katika sekta zote zinazohusu uchumi wa taifa isipokuwa zile za utumishi wa umma. ATE ina
jumla ya wanachama wa moja kwa moja wapatao 1500 waliosajiliwa na wengine zaidi ya 6000
wasio wa moja kwa moja wanaaotoka makampuni binafsi ya kibiashara na baadhi ya mashirika
ya umma.

Aidha zaidi ya mamlaka yake kuu ya kulinda maslahi ya waajiri na kuhakikisha mahusiano
mazuri baina ya waajiri na waajiriwa makazini, Chama cha Waajiri Tanzania pia kinahamasisha
na kuchochea mienendo mizuri ya usimamizi wa rasilimali watu na misingi bora miongoni mwa
waajiri ili kurahisisha uendeshaji wa biashara ambao ni muhimu katika uzalishaji na ushindani na
hivyo huandaa tuzo za waajiri kila mwaka ili kutambua na kuthamini makampuni yaliyofanya
vema katika kulinda misingi na mienendo ya usimamizi wa rasilimali watu.

Chama hutoa uanachama unaojumuisha makampuni makubwa, ya kati, madogo na madogo
zaidi kutoka sekta mbalimbali za uchumi wa taifa. Wanachama ni pamoja na makampuni binafsi
na ya umma, mashirika ya umma, vyama vya ushirika, balozi mbalimbali, vyama vya kibiashara,
taasisi za kidini, asasi binafsi (NGOs), na watu binafsi. Uanachama wa ATE upo kwa ajili ya waajiri
wote nchini Tanznia:- watu binafsi,vikundi, makampuni, mashirika ya umma, serikali za mitaa na
mamlaka zingine za nchi au vyama vya waajiri na kwa sasa chama kimegawanyika katika idara
8 ikiwemo kilimo, biashara, viwanda, ushirika na huduma, benki na fedha, madini, mafuta na
usalama binafsi.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na mratibu wa mradi wa tuzo za waajiri (EYA Project Coordinator)
Joyce Nangai kupitia +255 784 702670 au barua pepe nangai@ate.or.tz au wasiliana na Afisa
Mawasiliano (Communications Officer), Yunge Kanuda kupitia +255 657 453618 au barua pepe


kanuda@ate.or.tz

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages