A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, November 29, 2018

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WAJITOLEA DAMU KUCHANGIA WENYE UHITAJI

Mkurugeni Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza na waandishi wa habari akielezea jinsi wafanyakazi wa benki hiyo walivyoguswa katika kujitolea damu kwa ajili ya watu wenye uhitaji.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakijitolea damu ili kusaidia wenye uhitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Hazina na Masoko ya Fedha wa NBC, Peter Nalitolela akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu zoezi hilo. NBC imeandaa zoezi hilo kwa muda wa siku tatu ambapo wafanyakazi wake watashiriki katika uchangiaji wa damu kwa hiari.
Mmoja wa Wafanyakazi wa NBC, Salama Mussa (kulia), akipimwa damu yake ili kuona kama inakidhi vigezo vya kujitolea damu katika hafla hiyo. Anayempima ni mhudumu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Ndonya Hussein.
Mmoja wa wafanyakazi wa NBC, Jeff Ndossa (kulia), akijitolea damu ili kusaidia wenye uhitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika hafla iliyoandaliwa na NBC jijini Dar es Salaam jana. Anayemtoa damu ni mhudumu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Ali Juma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages