A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, August 18, 2018

Simba tena habari ya mjini yaitwanga Mtibwa Sugar

Leo Agosti 18 klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kutetea taji lake la mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu, Ngao ya Jamii kwa kuifunga Mtibwa Suger ya kutoka mkoani Morogoro kwa jumla ya mabao 2-1 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Elly Sasii aliyesaidiwa na Hellen Mduma wote wa Dar es Salaam, na Ferdinand Chacha wa Mwanza, hadi mapumziko Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-1.

Mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere alianza kuifungia Simba SC dakika ya 29 kwa shuti kali kutokea pembezoni mwa Uwanja kushoto, baada ya kuwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar na kipa wao, Benedictor Tinocco kufuatia kazi nzuri ya Hassan Dilunga.

Kelvin Sabato Kongwe au Kiduku akaisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 33 baada kupokea pasi nzuri ya Saleh Hamisi na kufumua shuti zuri akiwa anatazamwa na mabeki wa Simba SC.

Wakati refa Sasii anajiandaa kupuliza filimbi ya kukamilisha kipindi cha kwanza, Hassan Dilunga akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya dakika 45 stahili za mchezo.

Dilunga aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar mwezi uliopita tu baada ya awali kuchezea Ruvu Shooting, Yanga SC na JKT Ruvu, alifunga bao hilo kwa shuti lililowababatiza wachezaji wengine kufuatia pasi ya Mganda, Emmanuel Okwi.

Kipindi cha pili mchezo uliendelea kupendeza, Simba SC wakisaka mabao zaidi na Mtibwa Sugar wakitafuta bao la kusawazisha lakini hakuna timu iliyofanikiwa kutikisa nyavu.

Mtibwa ilipata pigo baada ya kiungo wake, Awadh Juma kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake imechukuliwa na Juma Luizio dakika ya 63, wote wamewahi kuchezea SImba SC.

Nahodha wa leo wa Simba SC, Emmanuel Okwi naye akashindwa kuendelea na mchezo dakika ya 66 akimpisha Nahodha wa klabu, John Bocco.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Nicolas Gyan, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dilunga/Muzamil Yassin dk78, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi/John Bocco dk66 na Shiza Kichuya/Shomari Kapombe dk73.

Mtibwa Sugar: Benedict Tinoco, Rogers Gabriel, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Hassan Isihaka, Shaban Nditi, Ismail Aidan, Salehe Hamis/Ally Makalani dk 85, Kelvin Sabato, Awadh Juma/Juma Luizio dk63 na Salum Kihimbwa/Haroun Chanongo dk73.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages