A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 14, 2018

Waziri Ummy atoa Ufafanuzi kuhusu Upimaji wa UKIMWI bar kwa bar



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema utaratibu wa upimaji wa kifua kikuu na UKIMWI bar kwa bar sio wa lazima, ila watatumia ushawishi kuhakikisha wananchi wanapima na kujua afya zao.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi (NACP).

”Tutatekeleza mpango wetu wa kupima TB na UKIMWI kwenye bar ila hautakuwa wa lazima, tutakachofanya ni kuwashawishi wananchi kutumia fursa ya kusogezewa huduma hiyo” amesema Ummy.

Aidha ameongezea kuwa Wizara ipo katika mkakati wa kubadilisha sera na sheria za UKIMWI na kuruhusu mtu aweze kujipima mwenyewe na kutoa fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kujipima wenyewe bila ridhaa ya wazazi.

Hatua hizo ni kufuatia serikali kutaka kubainisha na kuwatambua watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI pamoja na TB kauli ambayo ilitolewa Aprili 23 mwaka huu na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages