Mbunge wa viti maalum (CCM), Amina Mollel ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto ambao wana ulemavu kutowaficha bali wawape nafasi ya kupata elimu kwa kuwa ndiyo mkombozi wa maisha yao ya baadae.
Mbunge huyo amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii baada ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Nduruma na kuongeza kuwa hata yeye alipitia wakati mgumu kutokana na ulemavu wake ikiwemo kutemewa mate na wakina mama wajawazito kwa kuamini wanaweza kuzaa watoto wenye ulemavu kama yeye.
“Wakati nasoma wengi walinidharau na kuniona binti mwenye bahati mbaya kwa ulemavu wangu. Lakini familia yangu ilinipenda na wakaamini kuwa ni elimu pekee ndio mkombozi kwangu, wapo walionitema mate hasa wanawake wajawazito wakiamini wanaweza kuzaa mtoto kama mimi”, amesema Mollel.
Mbunge huyo aliongeza kwamba kila kitu kinawezekana jambo la msingi ni kuwa na malengo kwani mila na desturi za kimasai pamoja na ulemavu alionao angekua ameshaolewa katika umri mdogo na sasa angekuwa tayari ana wajukuu.
“Sasa ninaamini Mwenyezi Mungu alikuwa na sababu katika hili, inawezekana nilipomaliza shule kwa mujibu wa mila zetu Morani wangeshanioa na sasa ningekuwa na wajukuu haaaaaaaa. Olomuran enda suphai” ameongeza Mollel
Amina Mollel amewataka wananchi kuungana pamoja ili kuleta maendeleao kwani kwa sasa anafuraha kwa kuwa watu watatibiwa katika kituo cha kisasa na wakina mama watajifungua katika sehemu salama katika kituo cha afya cha Nduruma wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment