A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 24, 2018

Watanzania wawili kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kusoma na kuhifadhi QUR-AAN

Meya wa Wilaya ya Temeke  Abdallah Chaurembo (kushoto),akikabidhi Bendela ya Taifa kwa  vijana  Mbwana Abdala, kutoka Kaskazini pemba ( wanne kulia), na Shujaa Suleiman kutoka Morogoro, (wa kwanza kulia) kwaajili ya kwenda kuiwakilisha inchi katika mashindano ya Afrika yatakayofanyika jumapili ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kasasim Majaliwa, wanne kushoto ni Msimamizi wa Mashindano hayo Sheikh Nurdeen Kishk pampoja na viongozi wengine wa dini hiyo, Hafla hiyo imefanyika  viwanja vya shule ya Al-HIKMA  jijini hapa leo. 
 Msimamizi wa Mashindano ya kusoma na Kuhifadhi  Qur-aan Tukufu, Sheykh Nurdeen Kishk, (watatu kushoto)akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi Bendela ya Taifa kwa vijana wa kitanzania waliofuzu mashindano hayo kwaajili ya kwenda kuwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika, ambayo yatafanyika jumapili katika viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mh.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mh. Kasasim Majaliwa, (wa pilikushoto),  ni Meya wa Wilaya ya Temeke  Abdallah Chaurembo, (kulia) ni Mwenyekiti wa Mapambo  na ukumbi wa Mashindano hayo Haruna Jumanne, pamoja na Mwenyekiti wa Maulamaa wTanzania, Sheykh Suleyman Kilemile. Hafla hiyo imefanyika  viwanja vya shule ya Al-HIKMA  jijini hapa leo. 


Watanzania wawili leo Mei 24 wamekabidhiwa bendera ya taifa ili kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa ya 19 ya kusoma na kuhifadhi Qur-aan tukufu Afrika.

Akikabidhi bendera hiyo Meya wa manispaa ya Temeke Abdallah Chaulembo kwa wawakilishi pekee ambao ni Shujaa Sulemani kutoka Morogoro na Mbwana Dadi kutoka Pemba amesema kuwa imezoeleka mara nyingi bendera yetu wanakabidhiwa timu za mpira, lakini leo imekuwa tofauti kwa vijana hawa kupata fursa adhimu kama hii.

"Napenda kushukuru taasisi ya Al-Hikma kwa kuandaa mashindano haya ambayo yatakuwa chachu kwa watanzania kuonesha uwezo na kipaji cha kusoma na kuhifadhi Qur-aan tukufu" amesma Chaulembo

Pia ametoa wito kwa watanzania wote kufika uwanja wa taifa kwa wingi siku ya mei 27 mwaka huu kushuhudua mashindano hayo ambapo hakuna kiingilio chochote na mgeni rasmi anatarajia kuwa ni Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa.

Msimamizi wa Mashindano ya kusoma na Kuhifadhi  Qur-aan Tukufu, Sheykh Nurdeen Kishk,

Kwa upande wake msimamizi wa mashindano hayo Sheikh Nurdeen Kishk amesema kuwa washiriki wamepatika kihalali kutoka maeneo yote ya Tanzania kwani ulifanyika mchojo kwa bila upendeleo.

Aliongeza kuwa mashindano haya yatashirikisha nchi 16 kutoka bara la Afrika huku kuanzia kesho kukitarajiwa kupokea washiriki na wageni kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Uingereza, Uganda, Afrika Kusini, Saudi Arabia, Omani na Kenya.

"Katika kinyang'anyilo hicho mimi na wewe hatujui mshindi wa kwanza atakuwa nani na atatoka nchi gani ambae atapata kitika cha fedha kipatacho milioni 15 kikubwa Watanzania wote tufike siku ya tarehe 27 kuona nini kitatokea" amesema Sheikh Kishk



Nae Rais wa taasisi hiyo Sheikh Sharif Abdulkadir  ameipongeza Serikali kwa kitendo cha kulinda amani ya nchi kuonesha ushirikiana kuanzia hatua ya mwanzo hadi sasa kwani bila amani huwezi kuandaa mashindano kama haya na kupata washiriki kutoka nchi tofautitofauti kuja kushiriki. 
 Mwenyekiti wa Mapambo  na ukumbi wa Mashindano hayo Haruna Jumanne akizungumza katika hafla hiyo.
 Meya wa Wilaya ya Temeke  Abdallah Chaurembo akizungumza katika hafla hiyo
 Rais wa taasisi hiyo Sheikh Sharif Abdulkadir akizungumza katika hafla hiyo,

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages