Watu wasiopungua 25 wamefariki na wengine 27 bado hawajulikani walipo baada kimbunga cha Tropiki cha Sagar kusababisha mvua kubwa na mafuriko katika jimbo la Somaliland kaskazini mwa Somali.
Takwimu zilizotolewa zilionyesha kwamba zaidi ya watu 12 wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watoto kadhaa na kuna uwezekano idadi ya vifo kuongezeka.
Zaidi ya familia 167,250 zimeathiriwa na mafuriko hayo lakini operesheni za uokoaji bado zinaendelea.
No comments:
Post a Comment