A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 24, 2018

Steven Nyerere afunguka tuhuma za kusaliti ndoa yake


Muigizaji wa filamu bongo na mchekeshaji maarufu Steven Mengere maarufu kama Steve Nyerere, amefunguka juu ya tuhuma za kusaliti ndoa yake na kuzaa na muigizaji Wellu Sengo. Kitendo ambacho kimesababisha mke wake kuondoka nyumbani.

Akizungumza na www.eatv.tv, Steve Nyerere amesema kwamba yeye ni mwanaume rijali na kuzaa nje ya ndoa sio kitu cha ajabu, na mke wake wala hajaondoka kama watu wanavyodai kwenye mitandao ya kijamii

“Mke wangu yuko nyumbani, kakaa tuli katulia mtoto watu hana presha, kuna watu wangapi wamezaa nje!? Sasa mimi kwani sio mwanaume, kuna mwanaume mwenye kasoro duniani!? Labda shoga, mi ni mwanaume tena rijali, mwanaume ni yule anayeyimiza majukumu yake”, amesema Steve Nyerere.

Kutokana na hilo Steve Nyerere ametaka watu kuacha kujadili mambo yasiyo ya msingi kwenye mitandao ya kijamii na kueneza habari za uongo, na badala yake wafanye kazi kujiingizia kipato.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages