Zaidi ya makampuni 70 ya Ukandarasi yamejitolea kujenga mitaro katika barabara za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wataanza kujenga kwa maeneo yenye uhitaji wa kujengewa Mitaro.
Akizungumza katika mkutano na wakandarasi hao Mkuu wa Mkoa Mhe.Paul Makonda amewata wenyeviti wa serikali za mitaa kuratibu barabara zilizopo katika mitaa yao ambazo zinahitaji kuwekwa mitaro ambapo watachangia kwa baadhi ya mahitaji kama vile mchanga na Mawe.
Amesema kila mwenyekiti mwenye uhitaji baaa ya kuanishi maeneo yao watatakiwa kuonana na Mameneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini (TARURA) katika Wilaya zao ili wakutanishwe na wakandarasi hao.
Aidha amesema barabara nyingi zimekuwa zinaharibika kutokana na kukosekana kwa mitaro hivyo ujenzi huo utasaidia barabara kuwa katika hali nzuri hasa wakati wa mvua.
"Ninawashukuru sana wakandarasi waliojitokeza na ambao tayari wameanza kujenga mitaro na ambao amewaomba na wamekubali wote kwa Pamoja kujenga mitaro itakayowezesha maji kupita vizuri " Amesema Makonda.
Makonda Amewashukuru Makampuni ya Wakandarasi hayo waliojitokeza na kusema kuwa barabara ni muhimu kwa wananchi na inasaidia kurahisisha watu kufika katika shughuli zao ili kukuza uchumi wao binafsi na taifa kwa Ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Ibra Maida Waziri amesema kampuni hizo zitajenga mitaro yenye urefu wa mita 100 na kuwataka makampuni mengine kuunga mkono ujenzi huo lengo.
Amesema katika kuhakikisha barabara zinabaki katika ubora wake baada ya kuwepo kwa mitaro ili kuepusha ubovu wa barabara.
"Mimi na kampuni yangu tayari tumeshaanza kutekeleza miradi huu wa mitaro katika baadhi ya mitaa na maeneo mengine tayari tumeweka vifusi tunasubiri mvua ziishe ili tuanze kazi" Amesema Maida.
No comments:
Post a Comment