A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 16, 2018

RC MAKONDA: WALIMU NA WANAFUNZI WATAKAOFANYA VIZURI MKOA WA DAR WATAKULA MEMA YA NCHI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na walimu pamoja na wanafuzi wa shule ya sekondari Makumbusho alipokwenda kukagua ujenzi wa ofisi za walimu


Hili ndio jengo la ofisi za walimu shule ya sekondari Makumbusho,
Afisa Elimu Mkoa wa  Dar es Salaam akizungumza katika hafla hiyo.

Wanafunzi wa shule hiyo wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa.




Hili ndio jengo la ofisi za walimu shule ya sekondari shule ya Kasulu Ilala,

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda alipokwenda kukauga ujenzi wa ofisi za walimu Ilala

Kampeni ya Ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam imezidi kupamba moto ambapo baadhi ya ofisi ujenzi wake umekamilika kwa kiasi kikubwa tayari kwa kukabidhiwa.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi huo kwa baadhi ya shule, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema miongoni mwa shule zilizokamilika ni shule ya Kasulu Ilala, Shule ya Sekondari Makumbusho iliyojengwa kwa ufadhili wa ubalozi wa China waliojitolea kujenga shule tano kwenye wilaya zote za Dar es salaam.

Makonda amesema ndani ya ofisi hizo kutakuwa na Ofisi ya mwalimu mkuu, Mwalimu mkuu msaidizi, ofisi ya walimu wa kawaida, ukumbi wa mikutano, chumba cha kuhifadhi mitihani, vifaa vya michezo, chumba cha muhasibu, chumba cha kubadili nguo, mapokezi, bafu, vyoo, ofisi ya karani huku zikisheheni samani za kisasa kama viti, Meza, Makabati, AC, Feni na TV.

Aidha amesema mbali na kujenga ofisi za walimu pia atahakikisha shule zote za mkoa wa Dar es salaam zinakuwa na umeme pamoja na maji ya kutosha ambapo amepata wadau watakaochimba visima 50 kwenye shule zenye uhitaji.

Pia amewataka walimu kufundishwa kwa bidii na kwamba wanafunzi watakaofanya vizuri watapata zawadi nono sambamba na waalimu wao wa somo ambapo ametaka mkoa huo uongoze kwa kutoa wanafunzi bora na shule kumi bora kwa Ufaulu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages