Katika kuelekea Uchumi wa Viwanda Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imeandaa Maonyesho ya Wajasiriamali WakinaMama na Vijana wa Wilaya hiyo ambapo inawapa Fursa Wajasiriamali mbalimbali kushiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kutangaza biashara zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema maonesho hayo ni bure ambapo yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja yaliyoanza Jana na yatakayomalizika mnamo Mei 19, mwaka huu.
"Halmashauri ya Manisipaa ya Ilala imekuwa ikitekeleza majukumu yake katika kuwawezesha, kuwaelimisha na kuwaendeleza wajasiriamali wadogo, wa kati, na wakubwa kupitia mpango bajeti uliopangwa na Halmashauri na kuwawezesha vikundi mbalimbali kujiendeleza ili kujikwamua kiuchumi.Amesema Mjema.
Amesema katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2014 ,2015,2017 hadi 2018 Ilala imekuwa ikitenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ili kuwawezesha wajasiriamali hao kuendeleza na kukuza mfuko wao ili kujikwamua kiuchumi ili kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda.
"Katika mpango huu wa kusaidia vijana jumla ya shilingi bilioni 1.8 tumekopesha kwa vikundi vya wanawake na vijana 2,978 ambapo kati yao vijana 8,482 na wanawake 6,906 walinufaika na mkopo huo na kuweza kufanya ujasiriamali"Amesema.
Aidha amesema changamoto katika jitihada mbalimbali za kusaidia vikundi vya wajasiriamali wengi hasa wadogo hushindwa kunufaika na mfumo huo ni kutokana na masharti mbalimbali na kushindwa kukidhi vigezo hivyo.
Mjema amesema kutokana na changamoto hizo wamezingatia maelekezo serikali ya awamu ya tano kupitia viongozi mbalimbali na kufanya maboresho ya mfumo huo ili kukidhi mahitaji ya wajasiriamali.
Amesema takriban wajasiriamali 15,000 ambao wapo katika vikundi vikubwa na vidogo wenye shughuli za pamoja na mmoja mmoja wamenufaika na mkopo huo na kuweza kujiendesha na kufanya shughuli zao kwa ubora.
Amewataka watu mbalimbali kutembelea maonyesho hayo na kujifunza pamoja na kujionea ujasiriamali unaofanywa na Wana Ilala .
No comments:
Post a Comment