MKALI wa Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya na mumewe, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, wamesema kuwa, wapo bize kwa sasa na wamekuwa wakikesha kumsaka mdogo wake Krish ambaye ni mtoto wa mwanamama huyo aliyezaa na mumewe wa awali, marehemu Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Ijumaa Wikienda, mastaa hao walifunguka kuwa, kwa kipindi hiki cha mvua ndiyo muda sahihi wa kusaka mtoto hivyo wanalifanyia kazi suala hilo kwa nguvu zao zote.
“Tupo bize kidogo, tunasaka mtoto maana si unajua watu wanaangalia matunda ya ndoa kwa jicho la tatu hivyo sisi tunaangaika na hilo sasa hivi,” alisema Dogo Janja.
Kwa upande wa Uwoya alisema kuwa, yeye kama mwanamke anatakiwa kumzalia mumewe mtoto na hivyo kwa hivi sasa yeye na mumewe wapo katika harakati hizo kwa sababu Krish ameshakuwa mkubwa.
“Mke lazima amzalie mumewe na mimi na mume wangu sioni tunachosubiri kwa sasa maana Krish ni mkaka mkubwa na anahitaji mdogo wake,” alisema Uwoya.
Stori: Imelda Mtema, Dar
No comments:
Post a Comment