Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Polepole amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli, ameridhia uamuzi wa kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.
Aidha Abdulrahman Kinana ambae alikua Katibu mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ameng'atuka nafasi yake aliyokuwa akiishika ndani ya chama hicho na CCM wameridhia ombi hilo rasmi.
Hayo yamewekwa wazi na taarifa zilizotolewa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole leo Mei 28, 2018 na kusema kwa pamoja wamemtakia mafanikio mema katika shughuli zake.
"Napenda kumshukuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na CCM itaendeleaq kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali ya chama kwa kadiri itakavyohitajika", imesema taarifa hiyo.
Kwa upande mwingine, Kinana wakati anatoa neno lake la kuwaaga wajumbe wa NEC amewasisitizia wajumbe hao na wana CCM kiujumla kudumisha umoja wa wanachama na chama cha mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment