Ukizungumzia moja ya mameneja wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na Dansi hapa nchini, huwezi kuacha kutaja jina la Mohamed Kiumbe ‘Chief kiumbe’ jana amefuturisha jijini Dar es salaam katika ofisi za Respect Barber Shop Kinondoni ambapo mamia ya watu walihudhuria katika futari hiyo wakiwemo wasanii. mbalimbali wa bongofleva na filamu.
Pia Respect Barber Shop imeamua kuandaa futari hiyo kwa wakazi wa jiji hilo ili kuonesha upendo pia kama moja ya sadaka katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria Iftari hiyo ni pamoja na Khadija Kopa, Mwajuma Abdul ‘Queen Darling’ na Bonge la Nyau na wengine wengi wakiwepo wasanii wa dansi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Iftari hiyo, Msemaji wa saluni ya Respect, Dakota Delavida amesema kuwa huu ni mwanzo tu ila Mungu akiwapa uzima wataongeza wigo wao kwani ni kitendo cha kurudisha fadhila kwa jamii.
“Chakula ni sadaka na huwezi kupanga kiishie hapa tulijipanga vya kutosha, hii ni mara yetu ya kwanza mwenyezi Mungu akitujaalia uzima tutafanya tukio kama hili tena kwani ni kurudisha fadhili kwa jamii tunayoihudumia” alisema Dakota.
Wasimamizi wa shughuli hiyo wakiendelea kuhakikisha mambo yanakuwa sawia muda wote,
Msanii sheta akikaribia katika viwanja vya Respect Barbar Shop kwaajili ya kupata futari iliyoandaliwa na ofisi hiyo.
Msanii kutoka kundi la Tiptop Tunda Man akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Respect Barbar Shop kwakuandaa futari hiyo pia kama moja yakuwaweka watu karibu.
Dakota akigawa Chakula kwa wakazi waliohudhulia futari hiyo
Dakota akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Uongozi wa Respect Barbar Shop
Baadhi ya wasanii wa Dansi waliohudhulia futari hiyo
No comments:
Post a Comment