Mshambuliaji wa klabu ya Simba na kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara Emmanuel Okwi, amemwahidi Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson, kuwa ataendelea kushirikiana naye kuboresha elimu.
Okwi ameitoa ahadi hiyo leo baada ya kukutana na Naibu Spika Tulia Bungeni Dodoma, ambako timu hiyo ilipewa mwaliko maalum na Spika Job Ndugai baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2017/18.
Naibu Spika amesema, ''Leo nimefurahi sana kukutana na Balozi wa Mbeya Tulia Marathon 2018 mjini Dodoma, Mchezaji wa Soka Emmanuel Okwi, amekuwa Balozi mzuri na tunajivunia kuwa nae''.
Okwi kwa upande wake amemjibu Naibu Spika Tulia kwa kumshukuru na kumwahidi ushirikiano katika sekta ya elimu. ''Asante sana kwa imani yako juu yangu mama tuendelee kuboresha Elimu na Afya kupitia''. amesema.
Okwi ambaye ni raia wa Uganda amekuwa balozi wa taasisi ya Tulia Trust inayojihusisha na kusaidia wanafunzi kielimu pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo afya kupitia mbio za Mbeya Tulia Marathon.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, May 14, 2018
Okwi atoa ahadi hii kwa Naibu Spika
Tags
MICHEZO#
Share This
About kilole mzee
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment