Askofu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Njombe,
Isaya Mengele, amesema kuwa kitendo kilichofanywa na baadhi ya waumini
wa kanisa hilo Dayosisi ya Ziwa Tanganyika kumjeruhi kwa kumpiga mawe
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Tanganyika, Ambele Mwaipopo,limelitia doa kanisa hilo na kinapaswa kulaaniwa.
Akizungumza
jana katika ibada maalum iliyofanyika katika Kanisa la Kiaskofu la KKKT
Usharika wa Sumbawanga Mjini, Askofu Mengele ambaye ni Mwenyekiti wa
maaskofu wa KKKT Kanda ya Kusini, alisema ni aibu kubwa na fedheha kwa
dayosisi hiyo yenye miaka minne tangu kuanzishwa kwake na waumini hao
wanapaswa kutubu na kuomba radhi.
Alisema
kuwa pia yeye ataongoza ujumbe wa maaskofu wa kanda hiyo kwenda kwa
Rais John Magufuli kumuomba radhi kwa kitendo cha baadhi ya waumini hao
kuvuruga amani ambayo serikali yake imekuwa ikiihimiza kwa kitendo cha
kumjeruhi kwa kumpiga mawe Askofu Mwaipopo.
Pia
Askofu alimshauri Askofu Mwaipopo kuvunja Baraza la Dayosisi hiyo kwa
kuwa baadhi ya wajumbe wake wamekuwa ni chanzo cha mgogoro uliopo katika
kanisa hilo na wamekosa utii kwake.
Muda
mfupi kabla maaskofu sita wanaounda Kanda ya Kusini ya KKKT hawajafika
kuongoza ibada ya jana na kumpa pole Askofu Mwaipopo kwa kujeruhiwa,
baadhi ya waumini waliingia katika kanisa hilo na kuondoa kiti maalum
cha kukalia askofu huyo wakati wa kuongoza ibada.
Maaskofu
hao ni Renald Mtenji wa Ulanga Kilombero, Askofu Blastone Gaville
(Dayosisi ya Dira-Iringa), Askofu Job Mbwilo (Dayosisi ya Kusini
Magharibi- Matamba), Askofu Amon Mwenda (Dayosisi ya Ruvuma), Askofu
Edward Mwaikali (Dayosisi ya Konde Mbeya) na Askofu Isaya Mengele
(Dayosisi ya Kusini Njombe).
Lengo
la jopo hilo la maaskofu hao limefika kumpa pole Askofu Mwaipopo na
kuwasihi waumini waache mara moja vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kuwa
vinaliumiza na kulichafua kanisa hilo ambalo lina zaidi ya miaka 50
tangu kuanzishwa kwake nchini.
Katika
ibada hiyo Katibu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Fredrick Lazaro,
alisoma tamko maalum la Halmashauri Kuu kwa wakristo wa Usharika wa
Kathedral Sumbawanga Mjini kuekeleza waumini 21 na watumishi wa kanisa
hilo kuwa wamejitenga na kanisa hilo kwa muda usiojulikana.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk. Alfan
Haule, alisema vitendo vya uvunjifu wa amani havitafumbiwa macho na
serikali na kama vitaendelea, itatumia vyombo vyake vya ulinzi na
usalama kuvidhibiti.
Dk.
Khaule aliagiza kuwa wote walioiba kiti cha Askofu Mwaipopo wasakwe na
wakamatwe, ili wafikishwe mbele ya sheria wachukuliwe hatua kwani
kitendo cha kuiba kiti hicho ni wizi kama wizi mwingine wowote.
Mei
7, mwaka huu, Askofu Mwaipopo alifukuzwa kwa mawe baada ya baadhi ya
waumini kumzuia kuingia usharikani wakidai hawataki kumuona akiwepo eneo
la kanisa la Usharika wa Simbawanga Mjini.
No comments:
Post a Comment