Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Sylvester Ambokile , (kulia) akifurahia jambo pamoja na
Mmiliki wa mgahawa huo.
Msanii wa bongo fleva sheta akipiga msosi katika Mgahawa huo.
BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Sylvester Ambokile ,
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mgahawa wa kisasa wa chakula cha Kitanzania uitwao Grill House Take Away jijini Johanesburg nchini humo.
Mgahawa huo unalengo la kutangaza chakula asili cha kitanzania kimataifa
pamoja na kuwapa huduma hiyo watanzania waishio nchini humo.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, jana kwa
niaba ya Mmiliki wa Mgahawa huo ,
Christopher Robert, mwakilishi wa mkurugenzi huyo hapa nchini, Frank
Koko alisema sherehe za ufunguzi rasmi zimepangwa kufanyika Juni 21 mwaka huu.
“Dhima yetu ni kukitangaza chakula asilia cha kitanzania kimataifa.
Wapishi wote ni kutoka Tanzania na chakula kinasafirishwa kutoka Tanzania hadi
nchini humo,”alisema Koko.
Alisema, kwa miaka mingi chakula cha kitanzania hakijapewa nafasi kubwa
katika soko la hoteli na migahawa duniani kiasi cha kuwafanya hata watanzania wakiwa
nje ya nchi kulazimika kula chakula ambacho si asili yao.
“Tuliona kwamba hata hoteli za kitanzania zinapika zaidi chakula cha
utamaduni wa nje, watu wanalazimika kula tu.Ukifika Johanesburg ni
changamoto kubwa kupata chakula cha nyumbani.
Watanzania wanahangaika kupata chakula cha asili yao jambo ambalo
lilitusukuma kuja na wazo hili la kuwa na sehemu ambayo mtanzania akitua
Johanesburg atapata huduma zote kama za nyumbani,”alisema.
Aliongeza; “ Tunaomba watanzania watakaotembelea Johanesburg watemelee Grill
House Take Away , Mtaa wa
51 Regent ili
waweze kutuunga mkono,”alisema Koko.
Picha mbalimbali muonekano wa Mgahawa huo.
No comments:
Post a Comment