Mchekeshaji Mkude Simba amejibu hoja za Steve Nyerere kuhusu tuzo za za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF), huku akidai yeye si mchekeshaji.
Hapo awali Steve Nyere alihoji ni kwanini Ray, JB, Rich, Roams, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Duma, Weru, Hemedi, Tausi Mndengela, Mainda, Johari, Uwoya, Marian Ismail na Batuli hakushiriki tuzo hizo.
“Ambao movie tunazimiliki hatujauza haki zetu kwa muhindi ndio tuliweza kushiriki katika tuzo zile, lakini haimaamishi kwa wachekeshaji hote wawepo,” Mkude Simba ameiambia Bongo5.
“Hapana si hivyo, sijajua kuhusudio lake Steve Nyerere lakini huwa naamini mimi bado mchanga, bado najifunza kila siku. Mtu akiniambia mimi si mchekeshaji huwa nakubali na kweli mimi sio mchekeshaji ila nyuma yangu ndio kuna Bwakyila na Mkude Simba,” amesisitiza.
Tuzo za za Sinema Zetu International Film Festival Awards (SZIFF), zilitolewa April 01, 2018 ambapo muigizaji Gabo aliibuka na tuzo tano huku Wema Sepetu akishinda tuzo mbili.
No comments:
Post a Comment