Staa wa muziki kutokea Nigeria Davido ameweka hadharani kuwa hataki mpenzi wake Chioma apewe ubalozi kwenye kampuni yoyote kwa shillingi Milioni 60 atakubali tu kama deal hilo litakuwa la Milioni 100 na labda atafikiria kuhusiana na hilo.
Davido ameyasema hayo kupitia account yake ya twitter ambapo ameandika “Nimepata offer ya Milioni 60 za mradi wa mpenzi wangu lakini nimewaambia walete milioni 100 labda atafikiria”
Davido na Chioma inasemekana kuwa wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miaka mitano na pia kitu ambacho kilibeba headlines kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu Davido kumzawadia Chioma gari aina ya porshe lenye gharama zaidi ya shillingi milioni 200 kwenye birthday yake.
No comments:
Post a Comment