A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 3, 2018

Mama Kanumba apata mualiko Burundi

MAMA mzazi wa aliyekuwa staa maarufu wa filamu Bongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa juzikati ametimkia nchini Burundi kwa mualiko maalum aliopewa na wasanii wa kule ili kujifunza juu ya kazi zao za filamu walizofanya.

Akizungumza na Amani, mama Kanumba alisema kuwa baada ya kupata mualiko huo kutokana na wasanii hao kuthamini mchango wa marehemu mwanaye, ameona ni vyema kwenda na kitu nchini humo ambapo ataizindua filamu yake inayoitwa Capten Habona.

“Yani najisikia ni mtu ambaye ninaheshimika ingawa mtoto wangu hayupo hivyo filamu yangu hiyo nitazindulia huko kwa vile na wao wamenipa heshima kubwa sana kwa kuwa filamu yenyewe ina historia nzuri sana,” alisema mama huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages