UONGOZI wa klabu ya Simba SC umeitisha Mkutano wa mabadiliko ya
Katiba utakaofanyika Mei 20, mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere
uliopo eneo la Ocean Road mjini Dar es Salaam.
Mkutano huo umeitishwa na Kaimu Mwenyekiti, Salim Abdallah ‘Try Again’
ambaye amesema kwamba utaanza Saa 3:00 asubuhi na siku chache zijazo
wanachama wataumiwa ajenda kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya klabu hiyo,
kufungu cha nne.
Mkutano huo utafuatia ule wa Desemba 3, mwaka jana, ambao uliazimia
kumfanya mfanyabiashara Mohammed ‘Mo’ Dewji kuwa mwanahisa mkuu wa klabu
katika mfumo mpya wa uendeshwaji wa Simba SC.
Mo pekee aliweka dau la Sh Bilioni 20 kuomba asilimia 50 ya hisa, baada
ya klabu kutangaza kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa Sh. Bilioni 20
miezi miwili iliyopita, ingawa baadaye Serikali ikaagiza klabu hiyo
isiuze zaidi ya asilimia 49 kwa mtu mmoja.
Wanachama 1320 walihudhuria mkutano huo wa Desemba kutoka Dar es Salaam
na mikoa jirani na kwa furaha ya ushindi huo, Mo Dewji alitoa ahadi 10
za kuleta mabadiliko makubwa, ikiwemo ujenzi wa Uwanja wa mazoezi wa
nyasi za asili na nyasi bandia pamoja na hosteli ya kisasa ya wachezaji.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, May 3, 2018
Simba kufanya mkutano wa mabadiliko ya katiba Mei 20
Tags
MICHEZO#
Share This
About kilole mzee
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment