Mkuu wa Idara ya Habari na Mahusiano Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu,Kushoto Akipokea Pesa Taslimu kutoka Kwa Mkuu wa wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Manispaa hiyo Bi Benadetha Mwaikambo kulia, Katikati ni Muhasibu Idara ya Elimu Msingi Manispaa ya Ilala Bi Yasinta Andrew.
Na Mwandishi Wetu DSM.
Halmashauri ya Manispaa Ya Ilala jijini Dar Es Salaam,Kupitia Umoja wa Wanawake Watumishi wa Halmashauri hiyo Leo Mei 23 imeendelea na Zoezi la Kukusanya Michango ya kuwezesha Ujenzi wa Choo Cha Mtoto wa kike ikiwa ni Muendelezo wa ahadi zilizotolewa katika Harambee iliyozinduliwa Mapema mwezi Mei Mwaka huu.
Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea Vifaa pamoja na Pesa taslimu sh.Million Moja kutoka kwa Mchangiaji Benadetha Mwaikambo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Ilala, Afisa Habari ambaye pia ndio Muhamasishaji na Msimamizi wa harambee hiyo Bi Tabu Shaibu amesema Mpaka sasa hali ya michango inaendelea vizuri na kwamba Mafundi wanaendelea na Ujenzi wa Vyoo hivyo.
Kwa upande wake Bi Benadetha amesema amefurahi kuona amekamilisha ahadi yake ya kuchangia Sh. Million Moja kama alivyoahidi siku ya Harambee hiyo,na kuwataka watumishi wenzake hususani Wa Halmashauri ya Illala kujitahidi kumaliza Ahadi zao ili kufikia Malengo waliojiwekea.
Kampeni ya Ujenzi wa Choo cha Mtoto wa Kike ilizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Jophia Mjema tarehe 11 May 2018 ikiwa na kauli Mbiu isemayo "Binti Makini Mwamvuli wangu Stara," ikiwa na lengo moja la kumsitiri mtoto wa kike kwa kumpatia choo bora na chenye mazingira rafiki.
No comments:
Post a Comment