Blandina Chagula ‘Johari’
MKONGWE wa tasnia ya sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’, anadaiwa kuwa mjamzito wa miezi minne sasa ingawa mwenyewe amekuwa akificha.
Kwa mujibu wa sosi wa karibu wa staa huyo, kwa sasa Johari ameongezeka umbo kwa sababu ya ujauzito alionao ambapo anafurahia kwani ni jambo alilokuwa akilitafuta kwa muda mrefu.
“Mmemuona Johari kwa sasa? Ni mjamzito na mwenyewe ana furaha ingawa anaficha sana ili wapambe wasimharibie,” alisema sosi huyo ambaye ni mtu wa karibu wa Johari.
Baada ya ubuyu huo kutua kwenye meza ya Gazeti la Amani, mwanahabari wetu alimsaka Johari ambaye alimung’unya maneno na kudai kuwa yeye ni mwanamke hivyo hata akipata ujauzito si jambo baya na umri wake unaruhusu.
“Sipendi kuzungumzia hayo mambo yangu binafsi, kama mimba ipo mtaiona tu, lakini pia mimi ni mwanamke na umri wangu unaruhusu kuwa na ujauzito hivyo sioni tatizo,” alisema Johari.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Thursday, May 24, 2018
Johari adaiwa kunasa ujauzito
Tags
FILAMU#
Share This
About kilole mzee
FILAMU
Labels:
FILAMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment