A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 24, 2018

Ester afunguka kuteswa na Maruweruwe

Ester Kiama

MWANAMAMA anayefanya poa kwenye Bongo Muvi, Ester Kiama amefunguka kuwa, tangu akumbane na mkasa mzito wa kuleweshwa madawa ya kulevya amekuwa ni muoga hata kutoka ndani huku akiwa hamuamini mtu yeyote.

Akizungumza na Amani, Ester aliweka wazi kwamba, maruweruwe ya madawa hayajamuisha vizuri ingawa alishakwenda hospitalini na kupewa matatibu, lakini amekuwa na wasiwasi hata wa kununua chochote dukani kinachohusiana na majimaji.

“Huwezi kuamini kabisa, hata kutoka nyumbani kwangu ninaogopa sana, nimekuwa muoga kupitiliza na sijui hii hali  itaishaje kwa haraka, naona nimepata ugonjwa mwingine wa ajabu sana wa kuwa na wasiwasi,” alisema Ester.

Ester amekuwa katika hali hiyo baada ya juzikati kunyweshwa kinywaji chenye madawa ya kulevya na kuibiwa kila kitu alichokuwa nacho ikiwemo simu mbili na pesa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages