A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 24, 2018

Shamsa: Nimeamua kutulia na ndoa yangu


Shamsa Ford

STAA mwenye mvuto wa kipekee Bongo Movie, Shamsa Ford amesema kuwa, mambo yasiyo sahihi amefanya sana, lakini kwa sasa umefika wakati wa yeye kutulizana hasa kwenye ndoa yake.

Akichonga kiaina na Amani, Shamsa alisema kuwa, kutokana na kubadilika kitabia anatamani yeye na mume wake wawe mfano imara kabisa kwa jamii yaani waishi muda mrefu sana mpaka Mungu atakapowatenganisha.

“Maisha siku hizi ni mafupi sana, ni muhimu mtu siku ukiondoka uache alama nzuri na ili hilo lifanikiwe ni muhimu kutulizana, jambo ambalo nimeamua kulifanya kwa sasa,” alimaliza Shamsa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages