A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, May 26, 2018

Dini ya Beyonce YazuaGumzo Duniani


 MWAKA 1990 akiwa na umri wa miaka tisa, msanii wa Muziki wa R&B alijiunga kwa mara ya kwanza katika shule ya awali ya Parker Elementary huko Houston, Marekani.

Akiwa shuleni hapo ambapo pia hufundisha muziki, Beyonce alikuwa mmoja wa waimba kwaya wazuri. Miaka minne mbele, Beyonce aliteuliwa kuwa kiongozi wa kwaya katika kanisa waliokuwa wakisali wazazi wake la St John’s United Methodist.

Kuonesha kuwa muziki upo kwenye damu, katika kipindi hicho Beyonce alikutana na rafiki yake, LaTavia Roberson na kuamua kutengeneza kikundi cha wasichana cha kuimba na kucheza dansi kiitwacho Girl’s Tyme, hapo ndipo kukaibuka wasanii sita akiwemo Kelly Rowland.

Bada ya kupitia matamasha mengi, Girl’s Tyme waliamua kubadili jina la kundi na kujiita Destiny’s Child ambapo walibakiwa na wasanii watatu ambao ni Beyoncé Knowles, Kelly Rowland na Michelle Williams.

Ukiachilia mbali historia hiyo fupi ambayo baadaye kundi hilo lilikuja kugawanyika kila mmoja akifanya maisha yake. Kwa muda sasa Beyonce amefanikiwa kuiteka dunia katika burudani kupitia nyimbo zake, tangu alipoibuka na albamu yake ya kwanza ya Dangerously in Love (2003).

Maisha yanakwenda kasi sana! Beyonce ambaye kwa sasa ni mama wa watoto watatu aliozaa na Rapa Shawn Carter ‘Jay Z’ amekumbuka alipotoka, alipokuwa akiishi maisha ya kiroho, alipokuwa akiimba kwaya hadi kuwa kiongozi. Amekuja kwa mgongo mwingine wa kuanzisha dini yake iitwayo Beyism.

Ni dini ya kuabudu iliyoanzishwa rasmi na marafiki wa Beyonce mwaka 2014 mjini Atlanta, Georgia, Marekani ikiwa na kanisa lake liitwalo The National Church of Bey. Dini hii ni maalumu kwa kumuabudu Beyonce kama mungu wao.

Kwa mujibu wa kiongozi muanzilishi wa dini hii, Pauline John Andrews, alianza kwa kufungua tovuti ya kuwaita watu kujiunga nao ambapo alifanikiwa kupata wafuasi 12, ndani ya kipindi kifupi walijitokeza wafuasi wengine 200 kanisani hapo. “Ni dini halisi, inayoonekana kiroho, inayoongea, yenye mungu anayepumua, anayeonekana kila siku,” anasema Pauline.

Baada ya kuanzishwa mjini Atlanta, Dini ya Beyism imeendelea kutawanyika hadi katika Jiji la San Francisco, California, Marekani ambapo katika Kanisa la Grace wanamisa maalumu ya Beyonce.

Katika kanisa hilo linaloongozwa na Mchungaji Yolanda Norton, ambaye anatumia biblia ya Beyonce iitwayo Beyble katika mafundisho pamoja na nyimbo zake.

Tayari makanisa yanayomuabudu Beyonce yanatumia Biblia maalum ziitwazo Beyble. Inaelezwa kuwa, upo utaratibu wa kuchapishwa kwa biblia hizo nyingi zitakazoanza kupatikana duniani kote bure. Mbali na Beyble, makanisa yanayomuabudu Beyonce hutumia nyimbo zake kama sehemu ya kwaya na kila nyimbo ina maana yake.

Mfano nyimbo kama Pretty Hurt ni ya Kiroho, Drunk in Love ni ya Uhusiano na Upendo, Heaven ni ya Kifo, Blue ni ya Watoto, Grown Women ni ya Nguvu na Uhuru, Superpower ni ya Upendo na Nguvu, Mine ni ya Upendo, Partition ni ya Uhusiano na Upendo, Blow ni Uhusiano pamoja na No Angel ya Uhusiano na Mapenzi.

Hivi karibuni, Beyonce ameongeza wigo wa dini yake kwa kununua kanisa mjini New Orleans nchini Marekani lenye thamani ya dola za Kimarekani 850,000 (zaidi ya bilioni 1.7)

Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ, kanisa hilo lilijengwa mwanzo wa miaka ya 1900 ambapo linasemekana kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100 na limekuwa halitumiki kwa muda mrefu baada ya waumini wengi kufariki dunia.

Kanisa hilo la ukubwa wa futi za mraba 7,500 linasemekana haliko mbali anapoishi dada wa Beyonce, Solange. Tayari Beyonce amenunua mjengo wa kuishi karibu na kanisa lake.

Inaelezwa kuwa, Dini ya Beyism tayari ina waumini maelfu ambapo inaonesha baadhi ya wafuasi wa Beyism ni watu maarufu kama vile Kanye West, Mariah Carey, Rihanna, Nicki Minaj na wengineo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages