Msanii wa muziki Bongo fleva, Belle 9 ambae alikuwa kimya kwa muda mrefu bila kutoa hit yoyote amefunguka amefunguka kuhusu kuwa na ndo kama ndio chanzo cha kumkwambisha na kupotea katika game ya muziki.
Mwanamuziki huyo ambae leo ametoa video ya ngoma mpya ‘Dada’ amesema kuwa hamna kitu kama hicho ila kuna mabadiliko katika maisha yake ukilinganisha na hapo awali.
“Kwa kusumbua sanaa hapana, lakini maisha binafsi inakuchukua kidogo,”amesema Belle9.
“Kama kijana zaidi ni usiriazi na familia kwa sababu vitu vimebadilika, kabla ya kufunga kuna vitu nilikuwa sivifahamu sasa navifahamu,” amesisitiza.
Katika hatua nyingine amesema kuwa mwezi wa tisa anatarajia kutoa EP ambayo itakuwa na jumla ya nyimbo 9 ambapo hadi sasa nyimbo tatu tayari amesharekodi.
No comments:
Post a Comment