MKUU
wa wilaya ya Lushoto January Lugangika akizungumza katika kikao cha
Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Bumbuli ambacho kwa mara ya kwanza
kilifanyika eneo la makao makuu ya Kwehangara
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Bumbuli Peter Nyalali akizungumza katika kikao cha
robo ya mwaka cha Baraza la Madiwani kilichofanyika eneo Jipya la Makao
Makuu ya Halamshauri hiyo Kwehangala kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo Amiri Sheiza
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza akizungumza katika kikao hicho
kwa kuwataka wananchi kuwa wamoja kuhakikisha halmashauri hiyo inbapata
mafanikio kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauti ya Bumbuli Peter Nyalali
Mkurugenzi
wa Halmashauti ya Bumbuli Peter Nyalali kushoto akiwa na Mwenyekiti wa
Halma shauri ya Bumbuli Amiri Sheiza wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye
kikao hicho
MKUU
wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga January Lugangika amewataka madiwani
wa halmshauri ya Bumbuli kuhakikisha wanashiriki katika kukagua miradi
inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ili kuiepusha kujengwa chini ya
kiwango na hivyo kukosa tija kwa wananchi.
Agizo
hilo alilitoa juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la
Madiwani cha kawaida cha robo tatu kilichofanyika kwa mara ya kwanza
katika makao makuu mapya ya halmashauri hiyo eneo la Kwehangara.
Alisema
iwapo madiwani hao watashindwa kukagua miradi hiyo inatoa mwanya kwa
wakandarasi kushindwa kuitekeleza kwa viwango vinavyotakiwa hali
inayopelekea kukosa tija na thamani halisi ya fedha zinazotumika. “Ndugu
zangu madiwani hakikisheni mnakagua miradi ya maendeleo hili ndio
jukumu lenu la msingi kwani msipofanya hivyo ndipo wakandarasi wanafanya
miradi hiyo isiwe na tija na hivyo matokeo yake gharama inayotumika
inakosa thamani yake”Alisema DC Lugangika.
Aidha
pia alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Peter Nyalali kuweka
utaratibu mzuri kwa madiwani ili waende kukagua miradi inayotekelezwa
hususani miradi ya maji ambayo imekuwa ikihujumiwa kutokana na
wakandarasi”Alisema.Nay
kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli Amiri Sheiza
alisema wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwasaidia kuwatatulia mambo
mawili makubwa kwao kuyapatia ufumbuzi.
Alisema
suala la kwanza ni ujenzi wa Jengo la Halmashauri eneo la Kwehangara na
pili ni ufunguzi wa kiwanda cha Mponde katika mambo hayo ameonyesha
namna anavyotujali.“Hivyo
tunamuomba Mungu amuongezee hekima na busara katika kuiendesha nchi na
pia napenda kumthibitishia Rais kwamba wananchi, Baraza la Madiwani
pamoja na kupishana kifikra bado tupo pamoja kufanya kazi bila
kubaguana”Alisema.
Hata
hivyo alionya kuwa mtu ambaye ataanzisha vimaneno kuhusu suala hilo
watamchukulia hatua kali kwa sababu atakuwa hana nia njema na wananchi
wa halmashauri hiyo katika kuwaletea maendeleo.
“Nionyesha
mtu yoyote atakayeleta vimaneno kuhusu suala hili sisi hatutamvumilia
tutamchukulia hatua kali kwani wana Bumbuli na mbunge wetu sote pamoja
“Alisema.
No comments:
Post a Comment